JUKWAA LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Huduma za Afya ngazi ya jamii

Utangulizi

Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Ngazi ya jamii inahusisha shughuli za uelimishaji, uhamasishaji na kuishirikisha jamii kwa kushirikisha makundi mbalimbali ya jamii kama vile viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, wagaga wa tiba mbadala. Lengo likiwa ni kuwezesha jamii kuwa na uelewa sahihi juu ya maswala ya afya na kuchukua hatua stahiki.

Dira

Jamii yenye afya na ustawi bora ambao utachangia maendeleo ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa.

Makusudio

Kuwa na jamii yenye afya bora ili iweze kuchangia kwenye maendeleo ya jamii.

Malengo

Kuwa na nguvu kazi ya sekta ya afya yenye ustadi, maarifa na kujitolea kwa ajili ya kutoa huduma za afya ngazi ya jamii
Kuunga mkono huduma za afya ngazi ya jamii kwa kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali.
Kuongeza utoaji na utumiaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii ambazo zimeunganishwa katika miundo iliyopo katika ngazi zote.
Kuimarisha uwezo wa miundo na umiliki katika utoaji na uratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii.
Kuimarisha ushiriki wa jamii na Umiliki endelevu wa huduma za afya na ustawi wa jamii nzima.
Kuimarisha ushiriki wa sekta mbalimbali ili kushughulikia masuala yanayohusu afya na ustawi wa jamii

Muundo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Afya Ngazi ya Jamii - Wizara ya Afya (NCBHPCo)

Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii –TAMISEMI

Mratibu wa Elimuya Afya kwa Umma ngazi ya mkoa

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Afya Ngazi ya Jamii - Wizara ya Afya (NCBHPCo)

Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii –TAMISEMI

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#