Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Elimu ya Afya

Utangulizi

Uniti ya Mawasiliano ya Afya ni moja ya Uniti zilizo chini ya Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma cha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uniti hii ina jukumu la kuratibu afua za elimu ya afya zinazolenga mabadiliko chanya ya mila, desturi na tabia na kusimamia utekelezaji wake katika ngazi zote.

Dira

Kuwa na jamii yenye afya bora na ustawi ambayo inachangia kikamilifu katika maendeleo binafsi na ya nchi.

Dhamira

Kuwezesha utoaji wa huduma madhubuti za mawasiliano ya afya ambazo zinawezesha kukinga, kukuza, kutibu, kurekebisha na kudumisha afya.

Malengo

Kupitia na kuhakiki vielelezo vya uelimishaji na uhamasishaji jamii mabadiliko ya mila, desturi na na tabia zinazohusu afya
Kutoa mwongozo wa kimkakati na ushauri wa kitaalam kwa afua za uelimishaji na uhamasishaji jamii zinazolenga mabadiliko ya mila, desturi na tabia zinazohusu afya
Kuratibu shughuli za vitengo na program za Wizara ya Afya na wadau mbalimbali ili kuwa na mkakati wa pamoja
Kutoa miongozo na viwango vya ubora katika kubuni, kuandaa, kutoa, kufuatilia na kutathmini afua za uelimishaji na uhamasishaji jamii zinazolenga mabadiliko chanya ya mila, desturi na tabia zinazohusu afya
Kubuni, kuandaa, kutengeneza na kusambaza vielelezo vya kuelimisha na kuhamasisha jamii nyakati za dharura na majanga ikiwemo milipuko ya magonjwa
Kutoa mafunzo kwa mikoa, wilaya na wadau ,mbalimbali
Kufanya usimamizi shirikishi wa shughuli za uelimishaji na uhamasishaji jamii katika ngazi ya Mkoa na Wilaya
Kutoa mwongozo ili kuhakikisha viwango na taratibu za utendaji kazi zinadumishwa na kuzingatiwa
Kuimarisha uwezo wa waratibu wa Elimu ya Afya wa Mikoa na Wilaya kelezaji katika kupanga, kubuni, kuandaa, kuzalisha, kusambaza, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za uelimishaji na uhamasishaji jamii zinazolenga mabadiiko chanya ya mila, desturi na tabia zinazohusu afya
Kubuni, kuandaa, kuzalisha na kusambaza ujumbe na vielelezo vya kuelimisha jamii kulingana na Kalenda ya Matukio ya afya ya Kitaifa na kimataifa
Kutunza nakala laini na ngumu za vielelezo vya kuelimisha jamii vilivyoidhinishwa

Uniti

Majukumu ya Studio ya Redio na Televisheni
 • Uzalishaji na usambazaji wa ujumbe na vielelezo vya elimu ya afya kama vile vipindi vya Radio na Televisheni, matangazo ya Radio na Televisheni na machapisho mfano mabango na vipeperushi
 • Kupiga picha za mnato na video kwenye matukio mbalimbali kama vile mikutano, maadhimisho,uzinduzi na matamko
Majukumu ya Upitiaji na Uhakiki wa Vielelezo
 • Kupitia, kuhakiki na kuidhinisha vielelezo vya kuelimisha na kuhamasisha jamii vinavyoandaliwa na Wizara na wadau wake ili kuhakikisha ubora na viwango vinazingatiwa
 • Kutoa mwongozo ili kuhakikisha kwamba viwango na taratibu zilizokubaliwa zinadumishwa na kuzingatiwa
 • Kutunza nakala laini na ngumu za vielelezo vya kuelimishajamii vilivyoidhinishwa
Majukumu ya Uelimishaji na Ushirikishaji Jamii nyakati za Dharura na Majanga
 • Kuratibu na kuongoza kamati ya elimu ya afya na ushirikishaji jamii nyakati za dharura na majanga kwa ajili ya kujiandaa na kukabiliana na dharura na majanga
 • Kuratibu na kutoa mwongozo kwenye utekelezaji wa shughuli za uelimishaji na ushirikishaji jamii nyakati za dharura na majanga katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri
Majukumu Kazi za kituo cha huduma za simu cha afya
 • Kupokea simu zinazopigwa kupitia namba ya bure ya 199 na kutoa majibu kulingana na maswali na mahitaji ya mpigaji
 • Kutoa elimu ya afya
 • RKupokea mrejesho kutoka kwenye jamii
Majukumu ya Uniti ya Uchapaji
 • Kufanya uchapaji wa nyaraka, machapisho na vitendea kazi mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya Wizara, Taasisi na Jamii.

Muundo

Mkuu – HC&SBCC Programu
 • Msimamizi – Audio Visual Studio
 • Mratibu - SBCC & CRC
 • Kiongozi – RCCE
 • Msimamizi - Afya Call Center (ACC)
 • Msimamizi – Printing
Mratibu wa Elimu ya Afya-OR-TAMISEMI
Mratibu wa Health Promotion Mkoa - Sekta ya Afya
Mratibu wa Health Promotion Halmashauri - Sekta ya Afya

Nyaraka za Elimu ya Afya

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#