JUKWAA LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma

Utangulizi

Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kipo chini ya Idara ya Kinga – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ili kufikia lengo la kuchangia ustawi wa Taifa kupitia Elimu bora ya Afya kwa Umma, Kitengo kinaongozwa na Dira na Makusudio yanayowezesha utekelezaji wa majukumu hayo.

Dira

Kuwa na jamii yenye afya bora na ustawi ambayo inachangia kikamilifu katika maendeleo binafsi na ya nchi.

Makusudio

Kuhamasisha, kulinda na kurejesha Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuzingatia na mipango sahihi, uratibiwa na kutolewa kufikia maendeleo endelevu ya Afya ya Jamii.

Programu

Huduma za Afya shuleni

Huduma za Afya shuleni

Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Shuleni unajumuisha mikakati, shughuli na huduma...

Huduma za Afya ngazi ya jamii

Huduma za Afya ngazi ya jamii

Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Ngazi ya jamii inahusisha shughuli za uelimishaji, uhamasishaji na...

Elimu ya Afya

Elimu ya Afya

Uniti ya Mawasiliano ya Afya ni moja ya Uniti zilizo chini ya Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma cha...

Vitengo vidogo

Kitengo hiki kimegawanyika katika vitengo vidogo vidogo vitano ili kurahisisha uratibu wa shughuli za uelimishaji, uhamasishaji na ushirikishaji Jamii katika masuala mbalimbali ya Afya. Vitengo hivyo vidogo vidogo ni pamoja na: 

 • Kitengo kidogo cha Mawasiliano ya Afya na mabadiliko ya Tabia Jamii (Health Communication Unit)
  • Afya Call Center
  • Content Review Committee
  • Audio-Visual and Studio
  • Printing and Design
  • Risk Communication and Community Engagement subcommittee (RCCE)   
 • Kitengo kidogo cha Huduma za Afya Shuleni (National School Health Program, NSHP)   
 • Kitengo kidogo cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii (National Community Based Health Program, NCBHP)    
 • Vitengo vingine vidogo ni pamja na Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji (M&E) pamoja na Tehama (ICT)

Majukumu ya Kitengo

Jukumu kuu la kitengo cha Elimu ya Ufya kwa umma ni kuratibu shughuli zote za uelimishaji wa masuala mbalimbali ya afya kwenye jamii. Majukumu mengine ni kama ifuatavyo:

 • Kuandaa na kupitia Miongozo ya Huduma za elimu ya afya mara kwa mara kulingana na mahitaji ya jamii.
 • Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Miongozo ya uelimishaji jamii kulingana na será ya afya
 • Kuandaa na Kuhakiki ubora wa vielelezo na jumbe za afya zinazotumika katika kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya afya.
 • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Kanda na Wadau wengine ili kuboresha Huduma za Elimu ya Afya kwa jamii.
 • Kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na kukabiliana na magonjwa ya milipuko na majanga yenya athari kiafya.
 • Kuandaa, na kuratibu shughuli za utafiti zinazolenga kuboresha utoaji wa Elimu ya Afya na huduma za afya ngazi ya jamii.
 • Kuratibu maadhimisho ya afya ya kitaifa na kimataifa. Mfano; siku ya afya duniani, siku ya UKIMWI duniani, Siku ya Kifua Kikuu duniani, Wiki ya unyonyeshaji, siku ya Malaria, siku ya kutotumia tumbaku duniani n.k.
 • Kuandaa na kusambaza vielelezo mbali mbali vyenye jumbe zinazolenga kuboresha afya ya wananchi kwa kupitia vyombo vya habari kama redio, televisheni, magazeti na njia za asili

Historia ya Kitengo cha Elimu ya Afya Kwa Umma

Kitengo hiki kilianzishwa rasmi na Wizara ya Afya mwaka 1957 kikiwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya...

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#