Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Wawezeshaji

Wawezeshaji ni wataalamu waliopata mafunzo maalumu ya ujengeaji uwezo na kutambuliwa na Wizara. Wawezeshaji hawa wamejengewa uwezo na mbinu za uwezeshaji kwa Waratibu, Wataalamu wa Afya na Wahudumu wa Afya ya Jamii. Wawezeshaji hawa wanatumia miongozo na nyenzo zilizopitishwa na kuidhinishwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yao.

Uwezeshaji kwa waratibu

1. Moduli na Zana za Uwezeshaji

Wawezeshaji wa Waratibu watatumia moduli za aina tatu. Moduli hizo ni;

 • Moduli ya Uwezeshaji Elimu ya Afya,
 • Moduli ya Uwezeshaji Huduma za Afya Ngazi ya Jamii
 • Moduli ya Uwezeshaji Huduma za Afya Shuleni

Pamoja na Moduli hizi, wawezeshaji hawa pia watatumia zana mbalimbali ili kuwajengea uwezo waratibu hawa katika kutekeleza majukumu yao. Zana hizo zitajumuisha;

 • Vitabu
 • Miongozo
 • Fomu mbalimbali
 • Projector
 • Manuals
 • Laptop

2. Mbinu na Njia za Uwezeshaji

Uwezeshaji wa kuwajengea uwezo Waratibu utazingatia mbinu na njia za mawasilisho, mijadala, mazoezi, matembezi na maigizo.

3. Tathmini ya Maendeleo ya Uwezeshaji

Tathmini ya maendeleo ya uwezeshaji kwa Waratibu utazingatia mazoezi, mitihani, majaribio, maswali na majibu ya papo kwa hapo.

Uwezeshaji kwa wahudumu wa Afya ya Jamii

1. Moduli na Zana za Uwezeshaji

Wawezeshaji wa Wahudumu wa Afya ya Jamii watatumia moduli za aina tano ili kuwajengea uwezo wahudumu hawa katika kutekeleza majukumu yao katika Jamii. Moduli hizo ni;

 • Moduli ya Kwanza: Misingi ya Elimu ya Afya kwa Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii
 • Moduli ya Pili: Misingi ya Huduma za Uzazi, Mama na Mtoto kwa Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii
 • Modli ya Tatu: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii
 • Moduli ya Nne: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Yasiyoambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii
 • Moduli ya Tano: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Utapiamlo katika Jamii

Pamoja na Moduli hizi, wawezeshaji hawa pia watatumia zana mbalimbali katika kuwajengea uwezo wahudumu hawa. Zana hizo zitajumuisha;

 • Vitabu
 • Miongozo
 • Fomu mbalimbali
 • Projector
 • Manuals
 • Laptop

2. Mbinu na Njia za Uwezeshaji

Uwezeshaji wa kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ya Jamii utazingatia mbinu na njia za mawasilisho, mijadala, mazoezi, matembezi na maigizo.

3. Tathmini ya Maendeleo ya Uwezeshaji

Tathmini ya maendeleo ya uwezeshaji kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii utazingatia mazoezi, mitihani, majaribio, maswali na majibu ya papo kwa hapo.

E-Learning

Tembelea mtandao wa E-Learning unaotolewa na Wizara ya Afya

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#