Moduli hii inalenga katika kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii katika kuelimisha na kuhamasisha jamii ili waweze kupata huduma za afya na uzazi katika vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na mtoto. Moduli hii ndani yake kuna Moduli ndogo ndogo tano.
Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya magonjwa ya kuambukizwa na jinsi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi katika jamii. Hali kadhalika, Moduli hii ina Moduli ndogo ndogo saba.
Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya magonjwa yasiyoambukizwa na jinsi ya kuzuia na kudhibiti katika jamii. Ndani ya Moduli hii, kuna Moduli ndogo ndogo nne.
Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya utapiamlo na jinsi ya kuzuia na kudhibiti tatizo hilo katika jamii. Moduli hii ndani yake ina Moduli ndogo ndogo nne.