Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Huduma za Afya ya Jamii

Utangulizi

Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya ya jamii inahusisha shughuli za uelimishaji, uhamasishaji na kuishirikisha jamii kwa kushirikisha makundi mbalimbali ya jamii kama vile viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, wagaga wa tiba mbadala. Lengo likiwa ni kuwezesha jamii kuwa na uelewa sahihi juu ya maswala ya afya na kuchukua hatua stahiki.

Dira

Jamii yenye afya na ustawi bora ambao utachangia maendeleo ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa.

Dhamira

Kuwa na jamii yenye afya bora ili iweze kuchangia kwenye maendeleo ya jamii.

Malengo

Kuwa na nguvu kazi ya sekta ya afya yenye ustadi, maarifa na kujitolea kwa ajili ya kutoa huduma za afya ngazi ya jamii
Kuunga mkono huduma za afya ngazi ya jamii kwa kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali.
Kuongeza utoaji na utumiaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii ambazo zimeunganishwa katika miundo iliyopo katika ngazi zote.
Kuimarisha uwezo wa miundo na umiliki katika utoaji na uratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii.
Kuimarisha ushiriki wa jamii na Umiliki endelevu wa huduma za afya na ustawi wa jamii nzima.
Kuimarisha ushiriki wa sekta mbalimbali ili kushughulikia masuala yanayohusu afya na ustawi wa jamii

Uniti

Majukumu ya Mafunzo kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii
 • Kuratibu upatikanaji wa Wahudumu wa Afya ya Jamii pamoja na taarifa zao.
 • Kusimamia uwezeshaji kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii.
Majukumu ya Ushirikishaji na Uhamasishaji Jamii Afya
 • Kushirikisha Jamii katika kubuni, kuandaa na kutekeleza mikakati sahihi ya uhamasishaji Afya kwa umma.
 • Kuhamasisha Jamii kuzingatia kanuni msingi za Afya.
Majukumu ya Huduma za Afya kwa makundi mbalimbali
 • Kuratibu, kusimamia na kuwezesha huduma za Afya katika ya jamii.
 • Utoaji wa huduma za Afya kwa makundi maalumu.Mfano;
  • Katika nyumba za wazee.
  • Rehabilitation Services.
  • Community psychiartry and psychology
  • People with Diabilities

Muundo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Afya ya Jamii (NCBHPCo) - WAMJW

Mratibu wa Huduma za Afya ya Jamii-OR–TAMISEMI

Mratibu wa Health Promotion Mkoa - Sekta ya Afya
Mratibu wa Health Promotion Halmashauri - Sekta ya Afya

Nyaraka za Huduma za Afya ya Jamii

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#